Kim Kardashian: Tumbo linanisumbua

0
754

Kim Kardashian Shows Off Huge Baby BumpNEW YORK, Marekani
MKE wa msanii wa hip hop, Kanye West, Kim Kardashian, amesema kwa sasa tumbo lake linaanza kumsumbua kutokana na ujauzito wake wa mtoto mpya.
Kim anatarajia kupata mtoto wa pili huku mtoto wa kwanza akijulikana kwa jina la North, hivyo ujauzito alionao unaelekea mwishoni kupata mtoto wa pili.
“Nguo zangu nyingi kwa sasa zinanibana kutokana na tumbo kuwa kubwa, hiyo ni dalili ya kuwa mtoto anaendelea vizuri.
“Natarajia kuwa na mtoto wa pili muda wowote Mungu akipenda na nashukuru naendelea vizuri kiafya na mtoto mtarajiwa pia,” alisema Kim.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here