Mayunga Nalimi afiwa na mama

0
1319

mayungaMSHINDI wa shindano ya muziki la Airtel Trace Star, Nalimi Mayunga, amefiwa na mama yake aliyekuwa akiishi mkoani Tabora.

Katika ukurasa wake ya facebook msanii huyo alituma picha akiwa katika basi la kuelekea Tabora na maneno yalisomeka kwamba: “Mwenyezi Mungu tunakuomba utufanyie wepesi katika safari yetu hii kuelekea Tabora natuweze kumuhifadhi salama mama yangu inshallah na ninakushukuru kwa kila jambo unipangialo kwani ni wewe pekee unayejua kesho ya mwanadamu na hatima yake, mpokee mama yangu salama.”

Msanii huyo alipata dili la kwenda kwenye mafunzo na kurekodi wimbo chini ya usimamizi wa mwanamuziki  maarufu nchini Marekani, Akon lenye thamani ya zaidi Sh milioni 500.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here