23 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

PPAA yaendelea kutoa elimu kwa umma Sabasaba

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imeendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu, malengo pamoja na mafanikio yake kupitia Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Katika maonesho haya, wananchi, wazabuni, taasisi nunuzi pamoja na wadau wa sekta ya ununuzi wamepata fursa ya kujifunza zaidi kuhusu PPAA na majukumu yake.

Mapema leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Lilian Mbassy, alitembelea banda la PPAA katika maonesho hayo. Akiwa huko, Bi. Mbassy alipata fursa ya kuelezewa majukumu na malengo ya Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma na maafisa wa mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa maafisa wa PPAA, mamlaka hiyo ina jukumu la kusimamia na kuhakikisha kuwa taratibu za ununuzi wa umma zinazingatia sheria na kanuni, hivyo kulinda maslahi ya umma na kuhakikisha uwazi na uwajibikaji katika michakato ya zabuni.

Maonesho ya Sabasaba yameendelea kuwa jukwaa muhimu kwa PPAA kuelimisha na kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kufuata taratibu za ununuzi wa umma, pamoja na kutoa nafasi kwa wadau mbalimbali kuelewa kwa undani kazi na malengo ya mamlaka hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles