23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi yateketeza shehena za bangi  

NA JANETH MUSHI

JESHI la Polisi, Mkoa wa Arusha limeteketeza hekari tisa za dawa za kulevya aina ya bangi zilizokuwa zimepandwa shambani.

Taarifa ya kuteketezwa kwa bangi hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, DCP Charles Mkumbo, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisini kwake mjini hapa.

Alisema bangi hiyo ilikuwa imepandwa katika mashamba yaliyo eneo la Kisimiri juu, Wilaya ya Arumeru.

Kamanda Mkumbo alisema sambamba na kuteketeza bangi hiyo, waliteketeza pia gunia 267 ya bangi yenye uzito wa kilogramu 17,355, zilizokutwa kwenye baadhi ya nyumba za wakazi wa kata hiyo.

“Katika operesheni yetu iliyofanyika Juni 29 na 30 mwaka huu tukishirikiana na vyombo vingine vya usalama, tumefanikiwa kuteketeza shehena hiyo ya bangi.

“Pia tulikamata misokoto 1,400 ya bangi yenye uzito wa kilogramu 1.5, lakini hakuna aliyekamatwa hadi sasa kwa sababu wakazi wa eneo hilo walikimbilia milimani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles