26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi yamkamata mtuhumiwa mauaji ya walinzi

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linamshikilia mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mohamed Jumaa (37) mkazi wa Kariakoo kwa tuhuma za mauaji ya watu walinzi wawili wa Kampuni ya Forty Security na kujeruhi wengine watano kwa kuwagonga na gari kwa makusudi.

Akizungumza na  waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema tukio hilo limetokea jana Alhamisi, Agosti 26, 2021 majira ya saa 12:00 za jioni eneo la Tungi wilayani kigamboni katika kituo cha kuuzia mafuta cha JM Petrol na kuwataja waliouawa kuwa ni Eliakimu Moro na Sanko Bakari.

“Mtuhumiwa huyo alikuwa akidaiwa na Benki ya Access ambayo ilikuwa kesi ya madai namba 118 ya mwaka 2018, ambapo katika shauri hiyo alishindwa, akakata rufaa mara kadhaa akashindwa na ikaamriwa na mahakama aondoke kwenye eneo hilo na kulikabidhiwa kwa Benki ya Access.

“Benki hiyo ilifanya taratibu za kisheria na baadaye inadaiwa mtu anayefahamika kwa jina la Fahad Said Mohammed akawa ameshinda zabuni hiyo. Jana mtu huyo (Fahad) alikwenda eneo lile ambalo ameshakabidhiwa na benki, mtuhumiwa alikuja akadai achukue lori lake aina ya DAFF lenye namba T 176 CYP, baada ya hapo alitoka nalo nje.

“Lakini baada ya muda mfupi aliingia na lori lile kwa kasi wakati walinzi wakiwa wamefunga milango ya geti, na kuingia ndani kwa nguvu na kuwagonga walinzi hao ambao walifariki huku akijeruhi wengine watano katika tukio hilo. Mtuhumiwa amekamatwa na uchunguzi wa kina unaendelea, taratibu za kisheria zikikamilika atafikishwa mahakamani,” amesema Kamanda Muliro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles