24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Waliopata daraja sifuri ‘Mock’ kuwekwa kambi Simiyu

Na Derick Milton, Simiyu.

Jumla ya wanafunzi 2,098 wa kidato cha nne katika Mkoa wa Simiyu ambao wamepata daraja sifuri  katika mtihani wa utimilifu (Mock) mwaka huu, watawekwa kambi ya kitaaluma ya siku 60 ikiwa ni moja ya mkakati wa mkoa huo kufanya vizuri mtihani wa Taifa 2021.

Kambi hiyo pia itawajumuisha wanafunzi wachache takribani 50 waliopata daraja la kwanza kwenye mtihani huo, wakiwamo walimu mahili ambao watakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha wanapunguza daraja sifuri au kuzimaliza kabisa.

Mbinu ya kuwaweka kambi waliopata daraja sifuri kwenye mtihani wa utimilifu, imekuwa moja ya njia ambayo kwa muda wa zaidi ya miaka mitano imewezesha mkoa huo kufanya vizuri mtihani wa taifa na kuingia katika mikoa 10 bora kila mwaka.

Ofisa Elimu Mkoa Erenest Hinju, akitangaza matokeo ya mtihani huo leo ambao ulifanyika Julai 26, 2021 amesema kuwa wanafunzi hao wataanza kambi hiyo Sepetemba Mosi hadi 30, Oktoba 2021.

Amesema kuwa lengo la mkoa ni kuhakikisha unashika nafasi za juu tatu katika matokeo ya mtihani wa taifa kidato cha nne 2021 kama ambavyo mkakati unavyoelezea.

“Katika kambi mkoa uteua walimu ambao ni mahili na wanakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hawa wanaweza kupata alama D angalau masomo mawili tu ili waweze kuapata daraja la nne” amesema Hinju.

Ofisa Elimu huyo akizungumzia hali ya ufahulu wa mtihani huo, amesema kuwa licha ya mkoa kushindwa kufikia malengo yake, ufahulu umeongezeka kutoka asilimia 79.1 na GPA 4.0018 mwaka 2020 hadi asilimia 81.54 na GPA ya 3.9617.

Amesema kuwa malengo ya mkoa yalikuwa kupata ufahulu wa asilimia 96 au zaidi pamoja na GPA ya 3.2000, ambapo ameeleza kazi kubwa bado ipo katika kufikia malengo hayo mtihani wa Taifa.

Kwa upande wao wanafunzi wameeleza sababu ambazo zimesababisha kushindwa kufikia malengo, imetokana na kufeli masomo ya sayansi hasa upande wa mafunzo kwa vitendo kutokana na kutokuwa na maabara kwenye shule zao.

“Ukweli matoke siyo mazuri na Kama wanafunzi hatujapenda, lakini tatizo kubwa ni upande wa mafunzo kwa vitendo (Practical) ukiangalia shuleni kwangu hatuna maabara ndiyo maana tumefeli, tunaomba wadau na serikali kutusaidia eneo hilo,” amesema wanafunzi Elisha Robert.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles