POLISI Jimbo la Minnesotta, nchini Marekani, wamekanusha taarifa za uvumi kwamba msanii wa muziki nchini humo, Prince Nelson, alijiua.
Msanii huyo alipoteza maisha Alhamisi wiki iliyopita huku akiwa nyumbani kwake katika jimbo hilo, polisi wamefanya uchunguzi na kugundua kwamba msanii huyo hakujiua.
Taarifa kutoka kwa Jeshi la Polisi zilisema uchunguzi umekamilika na hakuna dalili za msanii huyo kujiua ila taarifa kamili zitatolewa baadaye.
“Uchunguzi umekamilika lakini majibu kamili yatawekwa wazi baadaye, lakini hadi sasa hakuna ukweli kwamba msanii huyo alijiua kama taarifa zilivyoenea,” alisema Martha Weaver, msemaji wa polisi.