20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Birdman ataka heshima Cash Money

birdman-williamsNEW YORK, MAREKANI

BOSI wa kundi la Cash Money, Bryan Williams ‘Birdman’, amewajia juu watu ambao wanalidharau kundi hilo na kulitia ubaya.

Kuna baadhi ya mashabiki walikuwa wanalisema vibaya kundi hilo kwamba bosi huyo anawanyanyasa wasanii wake na kusababisha wengine kulikimbia kundi hilo.

Kutokana na hali hiyo, msanii huyo amewataka wadau na mashabiki wa muziki kuliheshimu kundi na kudai kwamba wao hawana mchango wowote hadi hapo lilipofika.

“Nashangaa kuona baadhi ya watu wakishambulia Cash Money, hii haina maana yoyote kikubwa ni kuheshimu kazi za watu kila mmoja ana mambo yake ya kufanya hivyo sioni sababu ya kulizungumzia kundi na jina langu.

“Wasanii ambao wapo kwenye kundi wanafanya vizuri na wanaridhika na kile ambacho kinaendelea na ndio maana baadhi yao wapo,” alisema Birdman.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles