21.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa ataka Tamasha la Krismasi, Pasaka mikoa ya Kusini

MajaliwaNA MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amemwomba Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, kupeleka huduma hiyo katika mikoa ya Kusini kwa sababu wanakosa huduma ya neno la Mungu.

Kampuni ya Msama huandaa Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba mwaka huu na Pasaka linalotarajia kufanyika mwakani hapa nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema kwa sasa tamasha hilo limekuwa na nguvu kubwa ya kuhakikisha inahamasisha jamii katika mambo mbalimbali hivyo ni wakati wa mikoa ya Kusini kufaidika.

“Nimefarijika sana na namna kampuni ya Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake, Alex Msama, inavyofanyakazi zake katika kutoa burudani na kuelimisha jamii, kwa maana hiyo ningependa kuwaunga mkono katika hilo,” alisema Majaliwa.

Mikoa mingi ikiwamo Lindi na Mtwara nayo ina changamoto nyingi hivyo wanahitaji ujumbe kama unaotolewa katika Tamasha la Pasaka kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa,” alisema Majaliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles