24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI WAKAMATA WATUHUMIWA UPORAJI TAZARA

Na HERIETH FAUSTINE-DAR ES SALAAM


 

kamishna-simon-sirroJESHI la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia watu kadhaa kwa tuhuma za kuhusika na uporaji wa milioni 25 katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara.

Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon  Sirro, alikiri kutokea kwa tukio la uporaji huo ambapo alisema wamekamata watuhumiwa hao kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Kamishna Sirro alisema uporaji huo ulifanyika baada ya kuvunja kioo cha gari ndogo Toyota Rav 4 yenye namba T 455 DFN, mali ya Kampuni ya mabati ya Sun Share.

Alisema uporaji huo ulitokea juzi saa nne, wakati gari hilo likiwa kwenye foleni ya magari eneo la Tazara.

“Tukio hilo lilifanyika wakati gari hiyo ikiwa kwenye foleni katika taa za Tazara na halikuwa karibu na askari kama wanavyosema,” alisema Kamishna Sirro.

Aidha, aliongeza kuwa watu wanaosadikiwa ni majambazi wakati wa uporaji hawakupiga risasi juu ndio sababu iliyofanya askari kutojua kinachoendelea katika tukio hilo.

“Inaonekana hao watu walianza kuwafuatilia toka walipokuwa ila tumewakamata baadhi yao kwa ajili ya mahojiano huku upelelezi ukiendelea,” alisema.

Baadhi wa mashuhuda walisema wakati tukio hilo likifanyika kulikuwepo askari wa doria zaidi ya watano wakivurumushana na waendesha pikipiki upande wa barabara ya Mandela kutokea Buguruni.

Majambazi hao waliokuwa watatu walipora fedha hizo katika gari Toyota Rav4 yenye namba za usajili T544 DFN mali ya kampuni ya mabati ya Sun Share iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyejitambulisha Richard Charles.

Katika gari hiyo alikuwemo mfanyakazi mwingine wa kampuni hiyo mwenye asili ya China aliyetambulika kwa jina la Cheng Deng.

Kwa mujibu wa dereva wa gari hilo, Charles fedha hizo walikuwa wakipeleka katika benki eneo la Quality Center na ndipo walivamiwa na watu hao wakiwa na pikipiki aina ya Boxer wakati magari yakiwa foleni wakisubiri taa ziwaruhusu kupita kutoka barabara ya Mandela.

Charles alisema majambazi hao walimwamrisha kufungua mlango na kuwapatia begi la fedha lililokuwa limewekwa katika kiti cha nyuma huku wakimtishia kwa bastola kabla ya kuvunja kioo cha nyuma ya gari hilo na kubeba fedha hizo na kutokomea nazo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles