26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

ADAIWA KUTAPELI AKIJIFANYA MGANGA WA KIENYEJI

JOHANES RESPICHIUS Na BRIGHITER MASAKI (TSJ)-DAR ES SALAAM


 

vibuyuMKAZI wa Mapinga Bagamoyo mkoani Pwani, Twaribu Yusuph (34), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, akituhumiwa kutapeli fedha Sh milioni 60 akijifanya kuwa ni mganga wa kienyeji.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Obadi Bwegego, Mwendesha Mashtaka, Faraja Sambala, alidai mtuhumiwa huyo alifanya kosa hilo, Agosti 15, mwaka jana katika maeneo ya Bunju A, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo alimtapeli Sh milioni 60, Janeth Charles.

“Mtuhumiwa Twaribu ukiwa maeneo ya Bunju A jijini Dar es Salaam, ulimtapeli Sh milioni 60 Janeth Charles, ukijifanya mganga wa kienyeji, unaweza kumsaidia matatizo yake huku ukijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria,” alidai Faraja.

Mtuhumiwa alikana kufanya kosa hilo ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh milioni 30 kila mmoja kwa ajili ya kupata dhamana.

Kesi imeahirishwa hadi Januari 16, mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa amerudishwa rumande baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles