28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi wadaiwa kumshambulia ofisa wa Takukuru

Na GAUDENCY MSUYA-IKWIRIRI 

ASKARI  wa jeshi la Polisi wa kituo cha Ikwiriri Wilayani hapa, wanatuhumiwa kumshambujia na kisha kumjeruhi ofisa mmoja waTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), David Peter.

Ofisa huyo pia anadaiwa kuwekwa kituo cha polisi cha Ikwiriri tangu Alhamisi saa 5.00 usiku na hadi jana mchana alikuwa hajaachiwa.

Kwa mujibu wa habari zilizotolewa na walioshuhudia tukio hilo na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Rufiji, Onesmo Lyanga kuahidi kulitolea maelezo baadaye ni kwamba ofisa huyo wa Takukuru alishambuliwa saa 5.00 usiku wa kuamkia jana Ijumaa katika eneo la Ikwiriri Mgituti.

Mfanyabiashara wa mitumba wa Ikwiriri, Kaniki Amosi alisema aliona gari la polisi likisimama na baadaye askari wakaanza kumshambulia ofisa huyo wa Takukuru na kisha kumburuza hadi ndani ya gari na kutokomea naye.

Alisema baada ya gari hilo kusimama,ofisa mmoja  upelelezi wa Polisi Wilaya ya Ikwiriri alimuuliza David kwanini anagombana mara kwa mara na mkewe na alipoanza kujibu kwamba; ni vyema aitwe ofisini ili yafanyike mazungumzo, ndipo akaamuru askari wampige.

Kamanda wa kanda maalumu ya Rufiji, Onesmo Lyanga alisema atakapofikishiwa taarifa hiyo ofisini kwake atashughulikia haraka na kuchukua hatua kwa askari kama watakuwa wamefanya makosa.

“Hadi sasa taarifa hizo hazijafikishwa ofisini kwangu..hata hivyo baada ya kunieleza wewe nafuatilia ili nijue ukweli wa taarifa hizo kwa ajili ya kuchukua hatua na ninaahidi kwamba nitatolea ufafanuzi taarifa hizi kwa vyombo vya habari”alisema Kamanda Lyanga.

Mkurugenzi wa Takukuru Brigedia Jenerali John Mbungo alithibitisha kushambuliwa na kukamatwa kwa ofisa huyo wa Takukuru akisema ni ofisa wa upelelezi wa taasisi hiyo.

“Ni kweli ofisa wetu wa upelelezi ameshambuliwa na kukamatwa na polisi Ikwiriri tutatoa taarifa zaidi mara taarifa sahihi zitakapofika rasmi,” alisema Mbungo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles