20.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 5, 2022

Azam yafanya maboresho ving’amuzi vyake

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Azam imefanya maboresho kwa kuanzisha aina mpya ya visimbusi vya kidigitali (ving’amuzi ) vinavyotumia mfumo wa antenna ambavyo haviathiriwi na mabadiliko ya hali ya hewa ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Kulingana na utafiti uliofanywa na mtandao wa Brand Afrika juu ya ukuaji wa makampuni, kampuni hiyo imeshika nafasi ya tano miongoni mwa kampuni bora Afrika.

Akizungumza juzi Mkurugenzi Mtendaji Sabrina Mohamedali, alisema visimbusi hivyo ambavyo haviathiriwi na mabadiliko ya hali ya hewa, mteja anaweza akajiunganishia mwenyewe kwa wepesi na haraka zaidi.

“Kwa kupitia mfumo huu unaweza pia kupata chaneli za mkoa uliopo pamoja na chaneli nyingi zaidi za mataifa mbalimbali ya Afrika na dunia kwa ujumla,” alisema Sabrina.

Alisema visimbusi hivyo vitaanza kutumika Disemba Mosi na kwa kuanzia vitapatikana Dar es Salaam kisha mikoa mingine lengo likiwa ni kuwafikia wananchi wote.

“Tumekuja na teknolojia hii ya kisasa ili kutimiza malengo ya kuwafikia wananchi wengi kwa ubora kwa sababu visimbusi hivi haviathiriwi na mabadiliko ya hali ya hewa pia unaweza kukiweka sehemu yoyote kutokana na eneo lako kwa bei ya chini,” alisema.

Aidha alisema mbali na maboresho hayo wameingia mkataba wa ushirikiano na Wasafi TV na kwamba kuanzia Disemba Mosi chaneli hiyo itapatikana bila malipo ya ziada kama ilivyokuwa awali.

Alisema pia kutokana na maboresho hayo kuanzia Disemba Mosi kutakuwa ongezeko la chaneli na punguzo katika bei za vifurushi vyote.

Aidha alisema wameboresaha mitambo kuwezesha watazamaji kuziona chaneli kwa ubora zaidi na kwamba bei za vifurushi pia zitapungua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,686FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles