23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

UTAFITI: NIMR wabaini wenye VVU wengi wana kisukari

Na AVELINE  KITOMARY, DAR ES SALAAM

UTAFITI uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu(NIMR) umebaini kuwa wagonjwa wenye Virusi Vya Ukimwi (VVU) wanaotumia dawa wako hatari kupata ugonjwa wa kisukari.

Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalum, Mtafiti kutoka  Taasisi hiyo, Dk. Jeremia Kidole alisema utafiti huo ulihusisha watu ambao hawana virusi vya Ukimwi  655 na ambao wanavirusi vya Ukimwi wanaotumia dawa 656.

 “Huu ni utafiti ambao tulikuwa tunaangalia ukubwa wa tatizo la kisukari  katika wagonjwa ambao hawana virusi vya Ukimwi(HIV) na wale walivyonavyo  lakini hawatumii dawa na   wale wenye HIV ambao wanatumia dawa.

“Utafiti ulibaini kwamba wagonjwa ambao wana HIV na wanatumia dawa wako katika hatari ya kupata kisukari na wagonjwa ambao hawana HIV na hawatumii dawa wanahatari ndogo ya kupata kisukari.

“Tafiti hii imefanyika katika Mkoa wa Mwanza na imehusisha wagonjwa waliofuatiliwa kwa kipindi cha miaka 10 ni wagonjwa ambao alichukuliwa  mwaka 2005 mpaka 2009 na tukaja kuwaona tena mwaka 2017 hadi 2022,”alieleza Dk Kidole.

Aliongeza; “Hofu yetu ni kwamba hawa wagonjwa ambao  wana HIV na wako kwenye dawa wengi wao wanapata magonjwa ya kisukari na magonjwa mengi yasiyoambukiza. 

Dk. Kidole alisema hali hiyo hufanya  matibabu kuwa  mzigo kwa mgonjwa kutumia dawa kutokana na magonjwa hayo kuwa ya muda mrefu.

Dk. Kidole alibainisha kuwa katika utafiti huo walibaini kuwa ufanyaji mazoezi kwa wanaotumia dawa za VVU   hupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa  kisukari.

“Tukajaribu kuangalia ni vitu gani ambavyo tunatakiwa kufanya ili kupunguza tatizo  cha kwanza tukagundua  kuwa wale ambao ni HIV na wako kwenye dawa na wanafanya mazoezi hatari yao ya kupata magonjwa ya kisukari inapungua. 

“Katika kufanya hayo tukaamua kushauri serikali iweze kuingiza ‘component’ ya mazoezi kama mojawapo ya matibabu  ya HIV na kisukari  kwa wagonjwa kwasababu mazoezi ni kitu muhimu sana na kama itakuwa sehemu  ya matibabu kwa wagonjwa hao itasaidia kupunguza magonjwa yasiyoambukiza,”alieleza Dk Kidole. 

Pamoja na hayo alisema bado wanaendelea kufanya utafiti ili kubaini chanzo cha tatizo hilo kama dawa hizo zinasababisha tatizo  au virusi ndio sababu. 

“Kwa sababu tunaelewa upataji ugonjwa wa kisukari unahusishwa na kongosho kutokufanya kazi vizuri ambalo  linatoa vichocheo vya kupunguza kisukari sasa vile vichocheo visipotoka vya kutosha au vinaweza kutoka vya kutosha na vikashindwa kuunguza sukari au isitoke kabisa .

“Sasa tunataka kubaini kama vinatoka na havina nguvu tatizo ni nini ?na kama havitoki tatizo ni nini? Kwahiyo katika utafiti wetu wa awamu ya pili tutaliangalia hilo,”alifafanua Dk Kidole.

Aliogeza; “Kingine tunachofikiria ni  kwamba tunataka kuangalia kama ARVs ukitumia zinaongeza mafuta sehemu za tumbo na ukiwa na kitambi ni hatari ya kupata kisukari lakini pia  HIV yenyewe inaweza kwenda kwenye kongosho na kufanya vitu ambavyo vinabadilisha ule mfumo wa utengenezaji wa insulin. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles