25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi kuweni na utu kwenye utoaji haki-RC Mtaka

Na Derick Milton, Simiyu

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, amesema ili Mahakama iweze kutenda haki Kama Msingi Mkuu katika Utendaji kazi wake lazima vyombo vinavyohusika na ukamataji pamoja na upelelezi (Polisi) vitende haki pamoja na kuwa na utu katika hatua za awali za utolewaji haki.

Kiongozi huyo amesema kuwa wakati mwingine haki inakosekana kwa watuhumiwa kutokana na vyombo ambavyo vinahusika katika ukamataji na upelelezi kutotekeleza majukumu yao kwa haki pamoja na kutokuwa na utu.

Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo leo Jumapili, Januari 24, wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria na maazimisho ya miaka 100 ya mahakama nchini, ambavyo vimefanyika katika uwanja wa stendi ya zamani ya mji wa Bariadi.

Mtaka amelitaka jeshi la polisi kubadilika katika utendaji kazi wake, kwani haki ya mtuhumiwa uanza kupotea kwenye eneo lao kabla ya kufikishwa Mahakani hali ambayo watu wengi wamefungwa bila ya hatia.

Amesema kuwa malalamiko ya watu kusingiziwa na kubambikizwa kesi mbalimbali yamekuwa mengi ambapo jeshi la polisi limekuwa likilalamikiwa kwa tabia hiyo na kuwataka kubadilika ili haki iweze kutendeka.

“Ikiwa mkamataji na mpelelezi wakisema uongo, hapo hakuna haki hata kidogo, wala hakimu au mahakama inaweza kushindwa kupata ukweli ikaonekana uongo wa polisi ndiyo ukweli na mtu akapewa adhabu kumbe siyo kweli.

“Misingi ya haki na utu ianzie kwenye jeshi la polisi, hawa ndiyo wahusika wa awali kabisa kwenye kesi yeyote, Kama hivyo vitu havitakuwepo ni ngumu mtu myonge kupata haki, ni vyema polisi mkabadilika kwenye hilo,” amesema Mtaka.

Awali akizungumza kwenye uzinduzi huo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga, Gerson Mdemu amesema katika wiki hiyo watu watapata fursa ya kupewa elimu ya jinsi mahakama inavyofanya kazi kwa haki.

Jaji Mdemu ameongeza kuwa wamepanga kutumia wiki hiyo kuwafikia watu wote kwenye maeneo ya minada na magulio lengo likiwa kila Mtanzania kupewa elimu ya sheria pamoja na kutambua utendaji kazi wa muhimili huo wa nchi.

“Wananchi mnatakiwa kujitokeza kwa wingi kupitia maazimisho haya, kwa wiki nzima tutakuwa hapa Bariadi, tutakwenda kwenye minada na magulio, hivyo tunaomba mjitokeze kwa wingi mkapate elimu hii,” amesema Jaji Mdemu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles