24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Jiji la Mwanza kutumia Bilioni 13 kujenga soko

Na Sheila Katikula, Mwanza

Wafanyabiashara wa Soko la Kirumba wametakiwa kuwa wavumilivu wakati huu wa mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali nchini  kwani Soko hilo linatarajia kuanza kujengwa Julai, katika mwaka mpya wa fedha.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Kirumba, Wessa Juma aamese hayo wakati akizungumza na MtanzaniaDigital kwenye mahojiano maalum ofisini kwake kuhusu  hali ya miundo mbinu ya soko hilo.

Juma ambaye pia ni Diwani wa Kata hiyo amesema ujenzi wa soko hilo utagharimiwa na benki ya dunia Sh bilion 13 ambapo wakati huo Manispaa ya Ilemela inafanya taratibu za kutafuta mkandarasi atakayeshika kandarasi hiyo.

Amesema hatua za awali za kutafutia maeneo ya kuwahamishia kwa muda zinafanya ambapo alibainisha kuwa wafanyabiashara hao watahamishiwa  kwenye viwanja vya Magomeni, Furahisha na Ibanda pindi ujenzi utakapo anza kwani bado maeneo hayo hayajaanza kufanyiwa maandalizi na yanakabiliwa na changamoto ya miundo mbinu kama vyoo, maji na umeme.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko hilo, Elias Daudi alisema wakati huu serikali inapoteza fedha nyingi kwa sababu ya mvua zinazonyesha na kusababisha uhalibifu wa mali.

Alifafanua kuwa kuna baadhi ya bidhaa kama nafaka zinahalibiwa pindi mvua zinaponyesha  na kuingia ndani ya vibanda vya wafanyabiashara ukiachilia mbali wateja kushindwa kuingia ndani ya soko hilo kwa sababu ya kukosa seheme ya kungia kununua vitu na kupelekea mali kuhalibika sokoni.

“Serikali ikiboresha soko hili itasadia kuokoa fedha zinazopotea  pindi mvua zinaponyesha  na kuhalibu nafaka na vile vile tunaomba kama likijengwa tupewe kipaombele kwa wafanyabiashara wanaofanya  kazi zao tangu Siku nyingi na gharama za vyumba viwe rafiki kisiwe chanzo cha wao kufukuzwa kwa kutomudu gharama za pango,”amesema Daudi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles