25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Milioni 74 zilizotolewa kwa vikundi hewa Busega zachunguzwa

Na Derick Milton, Simiyu

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Simiyu imesema kuwa inachunguza kiasi cha Sh milioni 74.4 ambacho kilitolewa na halmashauri ya Wilaya ya Busega Mkoani humo kwa vikundi vya vijana, wanawake na walemavu ambapo baadhi ya vikundi vinadaiwa kuwa hewa.

Hayo yamesemwa juzi na Mkuu wa Takukuru Mkoa, Joshua Msuya wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Bariadi, ambapo amesema kuwa baadhi ya vikundi vingine wanufaika waligawana pesa.

Msuya amesema kuwa Halmashuari hiyo ilitoa kiasi hicho cha pesa kwa vikundi 23, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20, baadhi ya wanufaika hawakutekeleza shughuli ambazo waliombea fedha hizo na badala yake waligawana.

Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Simiyu Joshua Msuya akizungumza na waandishi wa habari juzi (hawapo pichani) ofisini kwake Mjini Bariadi.

Amesema kuwa katika uchunguzi wa awali wa fedha hizo baadhi ya vikundi ni hewa na havipo hivyo pesa hizo zilipelekwa kwenye vikundi ambavyo havipo, huku vingine ambavyo vilinufaika vikikutwa havina ofisi.

“Kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2020, tulipofanya uchunguzi, tumebaini kuwa wanufaika wamegawana fedha na shughuli walizoombea mikopo hazijatekelezwa,” amesema Msuya….

“Wengine hawana ofisi kabisa lakini walipewa mkopo, vikundi vingine ni hewa ila vinaonekana kuwa vilipewa mkopo, zoezi la ufuatiliaji na urejeshaji fedha linaendelea ikiwa pamoja na kufanya uchunguzi kwa vikundi hewa,” amesema Msuya.

Katika hatua nyingine taasisi hiyo inafanya ufuatiliji wenye lengo la kubaini jinai kwa wakopaji 10 kutoka wilaya za Meatu, Bariadi, Maswa na Busega ambao walikopa vifaa vya kilimo kutoka mfuko wa pembejeo Tanzania tangu mwaka 2006 lakini bado wameshindwa kurejesha mikopo hiyo.

Wakopaji hao wanadaiwa kukopa vifaa vyenye dhamani ya zaidi ya sh. Bilioni 1, ambapo licha ya mikopo hiyo kuwainua wakulima, urejeshwaji umekuwa na utata licha ya mfuko huo kufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha wanalipa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles