24.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 15, 2024

Contact us: [email protected]

POLEPOLE: TULIWAKATAA WABUNGE WA CHADEMA

SAFINA SARWATT Na OMARY MLEKWA-SIHA


KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (Itikadi na Uenezi), Humphrey Polepole, amesema nusu ya wabunge wa Chadema waliomba kujiunga na CCM kwa nyakati tofauti.

Hata hivyo, amesema baada ya CCM kutafakari maombi ya wabunge hao, waliamua kuwakataa kwa sababu hawana msaada wowote ndani ya chama hicho.

Polepole aliyasema hayo jana katika Kata ya Nag’arenairobi, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Siha.

“Karibu nusu ya wabunge wa Chadema waliomba kujiunga na CCM, lakini tuliwakataa kwa sababu wako sawa na mimba ya michongoma na ni mizigo na sisi hatuhitaji mizigo, tunataka vichwa.

“Chadema wajue kwamba, zile zama za kuendesha siasa za mihemko zimekwisha na sasa hivi ni zama za maendeleo. Pia wajue kwamba, tunawagonjea kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020 ili tuwaonyeshe majembe yetu ambayo ni vichwa japokuwa kwa sasa tunatesti mitambo yetu kwanza.

“Pamoja na hayo, ndugu wananchi wa Ngarenairobi nawaombeni mfanye uamuzi sahihi kwa kumpigia kura mgombea wa CCM ambaye ni Dk. Molel kwa sababu ndiye atakayeweza kutatua kero zenu,”alisema Polepole.

Naye Katibu wa CCM, Mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya, alivitaka vyama vya upinzani kushindana kwa hoja na siyo kutumia maneno ya vitisho.

“Kawaida yetu CCM ni kuendesha kampeni za kistaarabu ambazo wapinzani hawana. Kwa hiyo, nawaomba nao waige mfano wetu kwa kufanya kampeni za kistaarabu kwa sababu wananchi wamechoshwa na matusi bali wanataka kusikia sera na hoja,” alisema Mabihya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles