28.4 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Pinda amtaka Dk. Mwakyembe aongeze kasi

Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Na Khamis Mkotya, Dodoma

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amemtaka Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kuongeza juhudi katika kusimamia utendaji wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA).

Pinda alitoa agizo hilo jana wakati akiahirisha Bunge, ambapo alimsifia waziri huyo kutokana na jitihada zake za kupunguza muda wa kutoa mizigo bandarini kutokana na kuweka utaratibu wa kufanya kazi saa 24.

“Pamoja na changamoto zilizopo katika bandari zetu, napenda kutumia fursa hii kumpongeza Waziri wa Uchukuzi, Dk. Mwakyembe kwa kazi kubwa anayofanya,” alisema.

Pinda alikemea urasimu unaofanywa na baadhi ya watendaji bandarini, akisema kuwa vitendo hivyo vinakwamisha juhudi za Serikali za kuondoa malalamiko, hususan katika vituo vya forodha.

Pinda alisema baadhi ya watendaji wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakitumia vibaya taasisi mbalimbali zilizowekwa na Serikali, kama vile Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakala wa Viwango (TBS) na Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa (TFDA).

“Nimeelezwa kuwa baadhi ya watendaji wanatumia nafasi zao kuongeza urasimu usio wa lazima ili kudai rushwa, jambo ambalo linaongeza gharama kwa wafanyabiashara na kuleta athari za kuchelewesha utoaji wa mizigo.

“Naagiza wizara husika kufuatilia utendaji kazi wa vyombo hivyo kwa karibu na kushughulikia kwa haraka malalamiko mbalimbali na kupata ufumbuzi wa tatizo la urasimu katika vituo vya forodha,” alisema.

Hata hivyo, Pinda alisema utitiri wa makampuni ya forodha yapatayo 527 umekuwa chanzo kikubwa cha rushwa na ukwepaji wa kodi.

Alisema Serikali haitakubaliana na aina ya utendaji wa makampuni hayo na kutaka vitendo hivyo viachwe kwa kuviagiza vyombo husika kufuatilia kwa karibu mienendo ya makampuni hayo.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles