23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mgaya: Hii ni bajeti hewa

Nicolas Mgaya
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicolas Mgaya

NA ELIZABETH MJATTA
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Nicolas Mgaya, amesema tatizo linalokwamisha utendaji serikalini ni kitendo cha kusoma bajeti hewa huku fedha zikishindwa kupelekwa sehemu husika kwa ajili ya maendeleo.

Mgaya, ambaye alikuwa akizungumza na MTANZANIA Jumapili, alisema kwa miaka mingi wameshuhudia bajeti zikisomwa lakini kumekuwa hakuna mabadiliko yoyote.

“Bajeti inasomwa kila mwaka, lakini fedha haziendi kwenye wizara husika, hii inakuwa bajeti hewa kwasababu fedha zinatajwa kwamba zinakwenda kufanyia jambo fulani, lakini mwaka wa fedha unaofuata mambo yanakuwa yale yale, kunakuwa hakuna mabadiliko ya kile kilichosemwa, hii ni aibu kwa Serikali, ni lazima ibadilike,” alisema Mgaya.

Akizungumzia kushushwa kwa kiwango cha kodi ya Paye, Mgaya alisema Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani ameliongopea Bunge kwa kusema kuwa Serikali ilikutana na wafanyakazi na kukubaliana kiwango hicho kishuke kwa asilimia moja.

“Akiwa bungeni Celina Kombani amesema kwamba sisi tulikutana naye na tukakubaliana kiwango payee kishuke kwa asilimia 1 kwa maana kutoka asilimia 13 hadi 12, hii siyo kweli hata kidogo, hakuna sehemu ambayo tumekutana naye kujadili jambo kama hili.

“Tena afadhali angesema tuko kwenye mchakato kuliko kuliongopea Bunge, huu ni uongo mpana na hatari kwa taifa, Waziri amedanganya watu kupitia Bunge,” alisema Mgaya.

Mbali na hilo, Mgaya pia alisema kuwa wachumi wa hapa nchini wamekosa ubunifu kutokana na uwezo mdogo waliouonyesha wa kutegemea kuongeza kodi kwenye vyanzo vile vile kila mwaka.

Alisema kila mwaka bajeti ya Tanzania inategemea kuongeza ushuru kwenye vilevi, huku wakiacha vyanzo vingine, ikiwemo majumba ya kifahari yaliyoko katika Jiji la Dar es Salaam ambayo yanapangishwa kwa kodi.

“Wachumi wetu wanaotegemewa katika kuandaa bajeti wamechoka kufikiri, kila mwaka vyanzo ni vilevile, hakuna jipya kwenye bajeti, ukitegemea sigara na pombe kila mwaka uchumi utakua vipi,” alihoji Mgaya.

Alisema kwa sasa Jiji la Dar es Salaam watu wengi wanafanya biashara ya kupangisha nyumba, huku wengine wakitoza kodi kwa dola.

“Inashangaza kuona hapa Dar es Salaam kuna watu wengi wana majumba ya kifahari na wanatoza kodi kwa dola, lakini hawachukuliwi kama vyanzo vya mapato wakalipa kodi, bajeti kila mwaka inaegemea kwenye vilevi, huku ni kuchoka kufikiri,” alisema Mgaya.

Wakati akisoma bajeti ya fedha kwa mwaka 2014/2015 iliyopitishwa na Bunge la Bajeti mjini Dodoma, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, alisema ushuru umeendelea kupanda katika bidhaa za vinywaji baridi, vilevi pamoja na bidhaa za tumbaku kwa kila bidhaa moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles