26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Pilipili yamrudisha Matonya sokoni

Na GLORY MLAY

BAADA ya ukimya wa muda mrefu, nyota  wa muziki wa kizazi kipya, Seif Shaban ‘Matonya’, amerudi kwa kishindo na kutikisa anga ya burudani kwa wimbo wake mpya wa Pilipili.

Matonya ameweka wazi juu ya ukimya wake, akidai alikuwa amebanwa na mambo yake binafsi na kumfanya kupotea kidogo, akiwataka mashabiki wake kuendelee kumsapoti kwa kuwa amerudi upya.

“Mambo binafsi yananifanya nijiweke sawa katika maisha yangu, lakini mambo yote yametokana na kujihusisha na muziki, hivyo siwezi kuachana na muziki kwa kuwa ndio sehemu ya maisha yangu, nimerudi upya, mashabiki waendelee kunisapoti,” alisema Matonya.

Aliongeza kuwa mapokezi ya wimbo huo, yanaweza kumpa mwanga jinsi gani mashabiki wanamuhitaji sokoni, hivyo kujipanga kutoa wimbo mwingine mkali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles