29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dr Cheni jaji Miss Ilala 2019

NA JEREMIA ERNEST

MSANII mkongwe wa filamu nchini, Muksin Awadhi ‘Dr Cheni’, anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu katika usaili wa washiriki wa Miss Ilala mwaka huu.

Usaili huo utafanyika mwishoni mwa wiki hii katika hoteli ya Lamada, huku warembo 15 wakitarajia kushindana.

Akizungumza na MTANZANIA jana, mratibu wa shindano hilo, Lucas Rutainurwa, alisema usaili huo utafanywa kwa umakini ili kuwapata wawakilishi sahihi.

“Tutafanya usaili siku ya Jumamosi, Jaji Mkuu atakuwa Dr Cheni, huyu ni mdau mkubwa wa urembo hapa nchini, ataongozana na baadhi ya mastaa wengine ili kutenda haki,” alisema Lucas.

Aliongeza kuwa mwaka huu kamati yao imejipanga kuboresha zawadi, pia kumsaidia mrembo atakayepatikana kutwaa taji la Taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles