23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Piga utoboe kama Manula na Feisal

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya simu Infinix imewatambulisha rasmi wachezaji wa soka Feisal Salum almaarufu Fei Toto anaekipiga katika klub ya Yanga na na kipa wa klabu ya Simba, Aishi Manula kuwa mabalozi wa Promosheni ya PIGA UTOBOE.

Akizungumza Dar es Salaam Novemba 20, mwaka huu na Afisa Uhusiano wa Infinix, Eric Mkomoye ameasema kuwa Feisal na Aishi ni mabalozi wa kampeni hiyo sababu kapuni hiyo inathamini kijana mwenye kujituma kupitia kipaji.

Feisal Salum

“Kupitia Feisal na Aishi tunaamini vijana wengi wataTOBOA kupitia mbinu hizi.
“Hivyo kijana kupitia kipaji chako onyesha ufundi wa kupiga danadana kisha post na @infinixmobiletz na #PIGA UTOBOE na hapo utakuwa umejiweka kwnye nafasi yakujishindia Infinix NOTE 12.

“Au tembelea @infinixmobiletz bofya link kwenye BIO na utabiri mshindi wa kila mechi ya world cup na ushinde simu.Nunua Infinix NOTE 12, ZERO ULTRA, HOT 12 na ujishinde friji, TV inch 65, Pikipiki na GB 96 za internet na dakika 2,400 za maongezi kuzawadiwa papo hapo kwa mteja wa ZERO ULTRA,” amesema Mkomoye.

Aishi Manula.

Amesema kampeni hiyo inalenga kuwawezesha vijana wa Kitanzania na wateja wa kampuni hiyo kujizolea zawadi mbalimbali katika msimu huu wa Sikukuu ya Chrismass na Kombe la Dunia kwa kushiriki challenge mbalimbali kupitia @infinixmobiletz na kushinda zawadi kama Friji, Smart TV na Pikipiki.

“Vile vile katika msimu huu wa Chrismass na Kombe la dunia kupitia promosheni ya PIGA UTOBOE Infinix imeanza rasmi kufanya punguzo la bei kwa simu aina ya Infinix HOT 12 play kwa sasa inapatikana kwa bei ya jikoni kabisa na punguzo hili limeanza rasmi kwa simu zote, hivyo mteja anatakiwa kufika katika maduka yetu ili aweze kujioatia bidhaa hizi,” imesema Mkomoye.

Katika kampeni hiyo, kil wiki Infinix itatangaza washindi wa promosheni hiyo ambayo imeanza rasmi Novemba 19 hadi Januari 4.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles