25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 4, 2022

Contact us: [email protected]

Petit amtaka Wenger kung’atuka

Emmanuel PETITLONDON, England

MCHEZAJI wa zamani wa timu ya Arsenal, Emmanuel Petit, amemtaka kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger, kustaafu mwishoni mwa msimu huu na kuruhusu wenye uwezo wa kuiongoza timu hiyo kuchukua nafasi ya kufundisha.

Petit aliwahi kuwa kwenye timu ya Ufaransa iliyonyakuwa Kombe la Dunia mwaka 1998, pia alisajiliwa na Wenger akitokea Monaco na kusaidia kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England na FA mwaka huo.

Hata hivyo, Petit kwa sasa anahisi kwamba wakati umefika kwa Wenger  kuwa Mkurugenzi wa soka kwenye klabu hiyo ili kuongeza idadi ya wafuasi na kuijenga klabu hiyo na si nafasi ya ukocha.

Kauli hiyo iliungwa mkono na mchezaji wa zamani mwingine, Tony Adam na kudai kwamba baada ya miaka 20 ya mafanikio, Wenger anastahili heshima  katika klabu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,544FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles