22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kompany kuikosa Manchester United

Vicent KompanyLONDON, England

KOCHA wa timu ya Manchester City, Manuel Pellegrini, amethibitisha beki wa timu hiyo, Vicent Kompany, atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na jeraha la goti alilopata kwenye mchezo uliochezwa juzi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Dynamo Kiev.

Kompany amekuwa kwenye wakati mgumu msimu huu kutokana na majeruhi ya mara kwa mara baada ya kucheza michezo sita ya Ligi Kuu England.

Ingawa timu hiyo itamkosa mchezaji huyo kwenye michezo ijayo ukiwemo wa Manchester United, tayari imeweza kulinda nafasi yao na kuingia robo fainali  Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutoka sare ya 0-0 na kufanya matokeo ya jumla kuwa 3-1.

Pellegrini alithibitisha hilo baada ya kumalizika mchezo huo kuwa Kompany anaweza kuwa nje zaidi ya mwezi mmoja kutokana na majeruhi hayo.

Pia Kompany atakuwa nje kwenye mchezo dhidi ya Manchester United ambao timu hiyo inatakiwa kushinda ili iweze kuwa na matumaini ya kuwepo kwenye mbio za ubingwa msimu huu na robo fainali ya UEFA mwezi ujao.

Mbali na mchezo huo timu hiyo itakabiliwa na mchezo dhidi ya AFC Bournemouth, West Browm na Chelsea  utakaochezwa Aprili mwaka huu.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles