33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

PARIS KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA PANYA

Paris, Ufaransa


MEYA wa   Paris, nchini Ufaransa, Anne Hidalgo, ametangaza mipango ya kudhibiti ongezeko la panya katika jiji hilo.

Amesema atatumia   dola za Marekani milioni 1.6 kununua mitego mipya kwa ajili ya kunasa panya na kuongeza visahani vya kuwekea majivu ya sigara kwenye maeneo ya umma.

Inasemekana   wingi wa panya hao unakadiriwa kuwa kila mkazi mmoja anaweza kumiliki panya wawili.

Mwaka jana utawala wa mji huo ulifunga baadhi ya bustani za kupumzikia kama sehemu ya kupambana na panya hao.

Meya wa Paris amewataka pia wamiliki wa migahawa na majengo kuweka zaidi visahani vya kuwekea majivu kwa wavuta sigara.

Jiji la Paris linakusanya tani 150 vya mabaki ya sigara kila mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles