28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Pambano Simba na FC Platinum kupigwa saa 11

Na Richard Deogratious, Dar es Salaam

Afisa habari wa klabu ya Simba SC, Haji Manara ameelezea maandalizi yanayoendelea kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum itakayopigwa siku ya Jumatano, Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Manara amezungumza hayo leo Jumatatu, Januari 4,2021 kwenye kikao chake na waandishi wa habari katika hotel ya Serena Dar es Salaam.

Manara ameelezea juu ya mabadiliko ya muda wa mchezo huo kutoka saa 1 usiku hadi saa 11 jioni.

“Tunafurahi tumepokea majibu ya maombi yetu kwa Shirikisho la Mpira Barani Afrika (CAF), juu ya kuomba kurudishwa nyuma kwa muda wa kuchezwa hadi saa 11 jioni badala ya 1 usiku, kusudi letu likiwa ni jinsi ya kuwarudisha mashabiki wetu makwao kwani wengi wanatoka sehemu za mbali sana, hivyo ombi letu limekubaliwa na mchezo tutachezwa saa 11 jioni,” amesema Manara.

Pia Manara amewaomba mashabiki wa Simba pamoja Watanzania kuja kwa wingi Uwanja wa Benjamini Mkapa kuwa shangilia wachezaji na kuwapa hamasa kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho ili kuakikisha wanaibuka na ushindi.

“Simba ni timu ya watu na nguvu yetu ni mshabiki, hivyo mshabiki wetu mjitokeze kwa wingi kujaza Uwanja kwa asilimia 100, kwani tumeomba CAF tuzaje kwa asilimia 100 na kama watakubali tutaujaza Uwanja ila kama hawatokubali basi tutakwenda na asilimia 50 na kuujaza Uwanja wa Mkapa,” amesema Manara.

Aidha, Haji ameziomba na Klabu za ligi kuu bara kuwapa hamasa Simba, kwa kuwa Simba wakifuzu na taifa pia litakuwa na alama ambazo zilitaongeza ongezeko la timu nne kwa msimu ujao.

“Mimi nashangaa sana eti kuna mtu anaombea Simba kutolewa kwenye hatua hii, ila si jambo zuri kwani kufuzu kwa simba ni faida kwa Taifa kwani tutaridisha alama tulizoponywa na Libya ambayo haipo mwakani, hivyo tunaomba hamasa yetu ili tufuzu na tuongeze timu katika msimu ujao wa mashindano”. amesema Manara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles