25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Padri Kitima ataka viongozi wa dini kusimamia haki

ANDREW MSECHU

KATIBU wa Baraza la Maaskofu nchini (TEC), Padri Charles Kitima, amewataka viongozi wa dini kusimamia haki.

Akiongoza maadhimisho ya miaka 70 ya Azimio la Ulimwengu la Haki za Binadamu Dar es Salaam jana,  Padri Kitima alisema viongozi wa dini ndiyo wenye nafasi pekee ya kutoa mchango   kuhakikisha haki inapatikana.

Katika maadhimisho hayo yaliyokuwa na kaulimbiu “mchango wa dini mbalimbali kwa haki za biandamu Tanzania”, Kitima alisema ni wajibu wa viongozi  wa dini kusimamia ukweli bila woga hasa  wanapoona mambo hayaendi sawa na wakati mwingine wanalazimika kupata msaada wa  roho.

Alisema jamii inakabiliwa na  matatizo mengi yakiwamo ya wanandoa kuuana ovyo, unyanyasaji wa watoto wadogo na ukiukwaji wa makusudi wa sheria zinazosimamia haki za wengine, suala ambalo linastahili pia kusemewa bila woga.

Katika mkutano huo  uliowakutanisha viongozi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Jumuiya ya Wakristo Tanzania (CCT) na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Kitima alisema kutokana na nyakati kubadilika  viongozi wa dini wanapaswa kujikita kutatua kero za watu wao.

Akisoma kanuni za Azimio la Dunia la Haki za Binadamu, Gloria Makole kutoka Jumuiya ya Kikiristo Tanzania, Gloria Makole alisema miaka 70 ya Azimio hilo imekuwa chanzo cha ulinzi wa haki dhidi ya watu wanaojiona kuwa na haki kuliko wengine.

Alisema taasisi za dini zinapewa kazi ya kulinda, kutunza na kusimamia upatikanaji wa haki kwa  kufanya utafiti wa maeneo mbalimbali.

Mjumbe wa Baraza la Ulamaa (Bakwata-Dar es Salaam), Sheikh Issa Athuman alisema msingi mkubwa wa kuzungumzia haki za binadamu ni kumfanya mtu atambue kwanza thamani yake ndipo atakapojua haki zake.

  Joseph Ibreck kutoka TEC aliwataka viongozi wa dini kuangalia namna ya kuwasaidia hata viongozi wa siasa ambao ni sehemu ya waumini wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles