25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Padre mtarajiwa kizimbani kwa mauaji

Pg 3 sept 10NA JANETH MUSHI, ARUSHA

MTUHUMIWA wa mauaji katika Hoteli ya A Square Belmont jijini Arusha, Elijus Lyatuu (31), ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tano wa masomo ya falsafa katika Chuo cha Kanisa la Katoliki Segerea jijini Dar es Salaam, amepandishwa kizimbani na kusomewa shtaka la mauaji.

Mtuhumiwa huyo, alifikishwa mahakamani jana saa 4:30 asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi ndani ya gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili  PT 1434.

Mwendesha mashtaka wa Serikali, Lilian Mmasi, alidai mbele ya Hakimu Nestory Baro wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kwamba mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa la kumuua Alfred Kimbaa maarufu kwa jina la Mandela (18), Agosti 30, mwaka huu ndani ya Hoteli ya Belmont jijini hapa.

Alidai mtuhumiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 196 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Hata hivyo, aliomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutaja kesi hiyo kutokana na madai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

Kwa upande wake, hakimu Baro alimweleza mtuhumiwa huyo kuwa kesi inayomkabili haina dhamana, hivyo atalazimika kuendelea kukaa mahabusu hadi shauri hilo litakapoanza kusikilizwa.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba 23, mwaka huu itakapokwenda kwa ajili ya kutajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles