24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Samia: Msiuze kura zenu kwa bei ya chumvi

Pg 2 sept 10NA SARAH MOSSI, RUVUMA

MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, amewataka Watanzania kuthamini kura zao na kutokubali kuziuza kwa bei rahisi inayofanana na chumvi.

Samia, aliyasema hayo jana katika Kijiji cha Kingerikiti katika moja ya mikutano yake ya kampeni kwenye Jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma.

Akihutubia wananchi wa jimbo hilo, Samia alisema wapo watu wanaopita kuwahadaa kwa kutumia fedha ili wawapigie kura katika uchaguzi mkuu ujao, huku wakiahidi ahadi zisizotekelezeka.

Aliwataka wananchi kuwa makini na watu hao na kuhakikisha ifikapo Oktoba 25, mwaka huu wanafanya uamuzi sahihi.

Akiwa Kijiji cha Tingi, Samia aliwataka wananchi wa Jimbo la Nyasa kutokata tamaa na maendeleo yanayofanywa na Serikali licha ya jimbo hilo kuwa jipya.

Alisema ujenzi wa barabara katika jimbo hilo umeanza na utakamilika baada ya mgombea urais wa chama hicho, Dk. John Pombe Magufuli kuingia Ikulu.

“Dk. Magufuli ameshika wizara nyingi, anajua barabara zote na urefu wake… alipokuwa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, alijua mpaka idadi ya samaki,” alisema.

Alisema ili wananchi wa Nyasa na Mbinga Vijijini waendelee, Serikali imejipanga kuweka ajira kwa vijana kwa kujenga viwanda vikubwa na vidogo vya kubangua na kusaga kahawa na mahindi.

Katika kuwawezesha wananchi kiuchumi, alisema Serikali itajitahidi kuongeza pembejeo za kilimo ili itakapoweka viwanda viweze kuzalisha kwa wingi.

Akizungumzia sekta ya afya, aliwahakikishia wananchi wa Tingi kuwa kituo chao cha afya kitapandishwa hadhi na kuwa kituo cha afya cha wilaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles