Kocha mpya wa Simba raia wa Hispania, Pablo Franco  amewasili nchini leo Novemba 10,2021 tayari  kuanza kukinoa kikosi hicho.
Pablo mwenye umri wa miaka 41, amechukua nafasi ya Mfaransa, Didier Gomes aliyeachana na timu hiyo baada ya kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kibarua cha kwanza cha Pablo ataiongoza Simba katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting, huku akiwa na kazi ya kuhakikisha timu hiyo inatinga makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.