P Square wanusurika kifo Nigeria

0
1065

P-squareLAGOS, Nigeria

NYOTA wa muziki nchini Nigeria, mapacha wanaounda kundi la P-Square, Peter na Paul Okoye. wamenusurika kifo jana baada ya gari lao kugongana na lori la mizigo.

Ajali hiyo ilitokea katika mji wa Lagos, ambapo wasanii hao walikuwa katika gari aina ya Range Rover Sport SUV, lakini hata hivyo hali za wasanii hao zinaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu.

“Tunaamini Mungu yupo nasi kila wakati, ilikuwa ni ajali mbaya, ingeweza kutuondolea maisha yetu, lakini tunamshukuru Mungu ametulinda na sasa tunaendelea vizuri baada ya kupata matibabu,” waliandika wasanii hao katika kurasa za mitandano yao ya kijamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here