31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Efm kupeleka burudani ya muziki Mkuranga

3NA ASIFIWE GEORGE

KITUO cha redio Efm kesho kitaanza rasmi kampeni yake ya ‘muziki mnene, bar kwa bar’ katika Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani.

Meneja Mawasiliano wa Efm, Denis Ssebo, alisema mbali na burudani za muziki zitakazofanyika usiku na mchana, kutakuwa na mchezo wa mpira wa miguu ili kutoa nafasi kwa watakaoshindwa kujumuika nao katika burudani ya muziki unaofanyika usiku.

“Tutazunguka sehemu 12 katika wilaya tano kwa wiki 13, maeneo yatakayofikiwa ni Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe, Kibaha, Mlandizi, Kigamboni na maeneo mengine mengi na baada ya kuzunguka huko tutahitimisha kwa tamasha kubwa litakalofanyika jijini Dar es Salaam, safari hii limeboreshwa  na kuongezwa vionjo vingi vya burudani.

Naye meneja mwandamizi na mauzo wa kampuni ya simu za Smart, Haidari Chamshama, alisema msimu huu watazunguka na redio hiyo ya Efm wakiwa na bidhaa zao za simu zenye ubora wa hali ya juu ambazo wataziuza kwa bei nafuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles