29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

OUT yataka jitihada kukuza utalii

Na ELIYA MBONEA-ARUSHA

SERIKALI imetakiwa kutumia njia za kisasa zaidi katika kutangaza vivutio hivyo ili kuboresha huduma za utalii zitakazovuta idadi kubwa ya watalii   nchini,.

Changamoto hiyo imetolewa na wadau wa sekta ya utalii kwenye kongamano lililoandaliwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Kitivo cha utalii na kufanyika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) mkoani Arusha jana.

Kwa mujibu wa waandaaji wa kongamano hilo,   lengo ni kusaidia kukuza uelewa wa wadau wa utalii juu ya kuwapo na kuvitangaza vivutio vingine vilivyopo nchini tofauti na vilivyozoeleka hususan  wanyamapori.

Akizungumza kwenye kongamano hilo, Makamu Mkuu OUT, Profesa Elifas Bisanda,  aliwataka wadau wa utalii kuelekeza nguvu kubwa katika kuvitangaza vivutio vya utalii visivyofahamika kwa watu wengi.

“Tanzania ina vivutio vingi ambavyo havijafahamika kwa wananchi wenyewe na kwa watalii kutoka nje.

“Bado kuna changamoto kubwa kwenye eneo hili la kuvitangaza vivutio vya utalii visivyofahamika,” alisema Prof. Bisanda.

  Mkuu Kitivo Cha Utalii OUT, Dk. Felician Mutasa, alisema wanatarajia kongamano hilo litakuza uekewa kwenye eneo la vivutio vya utalii.

“Tunatarajia kongamano hili litapanua wigo wa huduma kwa watalii wanaoingia nchini na kuongeza idadi yao,” alisema Dk. Mutasa.

Akifungua kongamano hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Khamis Kigwangalla, alisema ipo haja ya kuwa na mpango imara wa kutumia teknolojia ya dijiti kutangaza vivutio vya utalii

“Kitendo cha kutangaza vivutio  kutasaidia kumudu ushindani mkali wa sekta hiyo katika mataifa na hatimaye kupata wageni wengi zaidi na kuongeza pato la taifa.

“Bado Tanzania haijafikiwa kujitangaza katika kiwango kinachotakiwa.

“Hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha  anakuwa sehemu ya kutangaza vivutio hivyo   viweze kujulikana kitaifa na kimataifa pia,” alisema Dk. Kigwangalla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles