22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

De Gea aingia matatani Man United

MANCHESTER, ENGLAND 

MASHABIKI wa Manchester United wamemjia juu mlinda mlango wao, David De Gea, baada ya kuonekana kwenye tangazo la pamoja na mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi, saa chache baada ya kufungwa na mchezaji huyo mabao mawili.

Tangazo hilo lilianza kuonekana muda mchache baada ya mapumziko ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, hatua ya robo fainali ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Manchester United kukubali kichapo cha mabao 3-0, mabao mawili yakifungwa na Messi na moja likifungwa na Philippe Coutinho.

Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 16 huku bao la pili likifungwa dakika ya 20 kabla ya Coutinho kufunga bao la tatu katika dakika ya 61, hivyo mashabiki wakashangaa kuona tangaza la UEFA ambapo Messi alionekana akiiba clips za De Gea.

De Gea ambaye anatajwa kuwa miongoni mwa walinda mlango bora duniani kwa sasa, alionekana kufungwa mabao rahisi kutoka kwa Messi hasa bao la pili, ambapo kipa huyo alionekana kama ameudaka mpira huo lakini kumbe ulimpita mikononi mwake.

Kitendo hicho kiliwafanya mashabiki kuhisi kama kuna mchezo umefanyika kati yake na Messi hasa baada ya kuonekana kwenye tangazo hilo.

“Kilichoonekana kwenye tangazo kimetushangaza wengi, tangazo limeonekana wakati wa mapumziko na tayari wakati huo Messi alikuwa amefunga mabao mawili, bao la pili lilikuwa rahisi sana kwa De Gea, kuna kitu kilifanyika kwa wawili hao.

“Inawezekana amechoka kuwa na Man United, hivyo ni wakati sasa wa kuachana na kipa huyo,” aliandika mmoja wa mashabiki kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Barcelona walifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya jumla ya ushindi wa mabao 4-0 kwa michezo yote miwili, hivyo wababe hao wa soka nchini Hispania wanatarajia kukutana na Liverpool katika hatua hiyo ya nusu fainali, wakati huo Ajax wakitarajia kukutana na Tottenham.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles