23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Othman kuongoza Timu ya ACT mageuzi ya kisiasa Zanzibar

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo upande wa Zanzibar, Masoud Othman Masoud ataongoza timu ya chama hicho kwenye majadiliano ya kukamilisha mageuzi ya kisheria ili kuimarisha haki, umoja na mshikamano.

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa na Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma, Salim Bimani leo Mei 19, 2023 imesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kikao cha majadiliano kilichohusisha viongozi wakuu wa chama hicho pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ally Mwinyi jana katika Ikulu ya Zanzibar jana.

Taarifa hiyo ya Bimani imesema Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya ACT Wazalendo waliokutana na Rais Dk. Nwinyi ni pamoja na Zitto Kabwe Kiongozi wa Chama, Juma Duni Haji Mwenyekiti wa Chama na Othman Masoud Othman ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar.

Bimani ameongeza kuwa viongozi hao walijadiliana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar hatua za kuchukua kukamilisha mchakato wa mageuzi ya kisheria yanayopaswa kufanyika Zanzibar ili kuimarisha Haki, Umoja na mshikamano.

Aidha amesema viongozi wa ACT Wazalendo wamemhakikishia Rais wa Zanzibar utayari wao wa kuharakisha mazungumzo ya vyama vikuu vya kisiasa nchini Zanzibar ambayo yatasaidia utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi cha Zanzibar kuhusu mageuzi ya kisiasa, kiutawala na masuala ya Uchaguzi.

“Ili kukamilisha suala hilo viongozi tayari wamewasilisha majina ya timu ya majadiliano ya watu sita (6) kutoka ACT Wazalendo kwa Rais wa Zanzibar itakayoongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Ndugu Othman Masoud Othman.

“Tunataka kuhakikisha kuwa vurugu na mauaji katika chaguzi inakuwa ni jambo la historia kwa Zanziba,r” alisema Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kuhusu mazungumzo yao na Rais wa Zanzibar.

“Tunaamini tutakubaliana kwa mambo yote ya msingi,” alisema Othman Masoud Othman kuhusu mazungumzo hayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Juma Duni Haji alitumia wasaa huo kumkabidhi Rais wa Zanzibar taarifa rasmi ya ACT Wazalendo kuhusu ukiukwaji wa Haki za Binaadam Zanzibar wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa ahadi yake ya kuitangaza na kuizindua Kamati hiyo wakati wowote kuanzia sasa.

“ACT Wazalendo kama taasisi inaunga mkono hatua ya viongozi wetu kukutana na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ikiwa ni utekelezaji wa azimio la Kamati Kuu na Kamati ya Uongozi Taifa na tunaahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kuhakikisha mchakato huu unatekelezwa kwa Maslahi ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla.

“Ni matumaini yetu kuwa kila mwenye kuitakia mema Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataunga mkono hatua hii na tunatoa wito kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kujitokeza hadharani kuonesha kumuunga Mkono Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia nia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,” ilieleza taarifa hiyo ya Bimani kwa vyombo vya habari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles