24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Bodaboda watakiwa kufuata sheria

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Bodaboda wametakiwa kufuata sheria za usalama barabara pamoja na kushiriki kwenye ulinzi wa raia na mali zake ili kupunguza uhalifu.

Akizungumza Mei 18, jijini dar es salaam wakati wa kikao cha ulinzi na usalam mtaa wa dovya kata ya Bunju mwenyekiti wa mtaa huo, Razalous Mwakiposya amesema matukio mengi ya uhalifu yakutumia bodaboda yanafanywa na bodaboda wenyewe hivyo jukumu la ulizi na usalam linawategemea wao

Amesema kuanzia sasa vijiwe vyote vya bodabado vinapaswa kusajiliwa ili kuwabaini wahalifu na visivyosajiliwa vitafutwa.

“Nitoe rai kwenu bodaboda vijiwe vyote visivyosajiliwa tutavifuta na pia hakikishine mnakua na utratibu wa kuwasiliana ukimuona mpya kwenye kijiwe chenu mumuhoji mkishindwa ripotini kwangu au kwa jeshi la polisi,”amesema Mwakiposya.

Nae Kamanda polisi Mkoa wa kipolisi Kawe, Deus Shatta amesema kuwa watashirikiana vizuri huku akitoa rai kwa madereva hao kuripoti matukio ya kiharifu kwani mtoa taarifa atalindwa.

Amesema kuwa madereva wa bodaboda wanapaswa kuwasafirisha abiria kwa aman na sio kuwadhalilisha

“Kumekua na udhalilishaji unaofanywa na bodaboda hasa kwa watoto mnapewa watoto muwapeleka shule lakini mnawageuka na kuwaingilia kingono sio vizuri na nakemea vikali zipendeni kazi zenu kwan hiyo ni kazi kam kazi nyingine,” amesema Kamanda Shatta.

Nae Mkuu wa Usalama Barabarani, ASP Rosemary Kitwala amesema uhalifu mwingi unatokea kutokana na mmomonyoko wa maadili na watu kukosa hofu ya Mungu hali inayopele uhalifu kuongezeka kwa kasi.

“Jamni turudi kwenye maadili hasa nyinyi vijana wa bodaboda mambo mengi yanatokea kutokana na nyinyi ndio maana hata mnashindwa kufuata sheria za usalama wa barabarani,” amesema Rosemary.

Aidha amesema kuwa bodaboda asie fuata sheria za usalama barabarani atachukuliwa hatua huku ametoa siku 10 kwa bobaboda wa kata ya dovya kuwa na kofia ngumu,refrector pamoja na kusajiliwa.

Nae Mkuu wa kituo cha Mbweni OCS Alex Buchuma ametoa rai kwa kwa wananchi kutii sheria bila shuruti kwani si lengo la polisi kumshurutisha mwananchi

Amesisitiza OCS ALEX bodaboda kuto chukua sheria mkononi pindi unapotekea uhalifu badala yake kutoa taarifa kituo cha polisi tukio hilo na kutoondoka eneo la tukio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles