24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 28, 2022

Orijino Komedi kutunisha mfuko wa Imetosha Foundation

orijino komediNA MWANDISHI WETU

USHIRIKIANO wa Imetosha Foundation na Orijino Komedi, unatarajia kutoa burudani ya vichekesho vyenye lengo ya kuchangisha fedha za ujenzi wa kituo kitakachoendesha shughuli za ujasiriamali kwa watu wenye ualbino.

Burudani hiyo kwa ajili ya kuchangia kituo hicho kitakachoitwa Santa Lucia ambacho kitajengwa huko Bumbuli Lushoto mkoani Tanga, itafanyika Septemba 11 katika usiku maalumu uliopewa jina la Ucheshi na muziki katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mmoja wa viongozi wa ushirikiano huo, Henry Mdimu, kituo hicho kitakuwa na shule na shughuli za ujasiriamali zitakazosaidia kuleta utayari wa kukataa dhana ya ulemavu na kuukwepa unyanyapaa dhidi yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,551FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles