Miss Albino kupatikana Septemba 4

0
656

AlbinoJULIET MORI, TUDARCO

SHINDANO la kumsaka mrembo wa watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Miss Albino’ linatarajiwa kufanyika Septemba 4 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo limeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Save Vulnerable Foundation (SVF) kupitia Baraza la Sanaa nchini (Basata).

Mratibu wa tamasha hilo, Fatuma Mjungu, amesema tamasha hilo linalenga kuibua na kutambua vipaji, kujenga ujasiri, kuwawezesha kufikia malengo yao, kuwajenga kiafya, kiuchumi na kielimu.

“Pia katika shindano hili tunatarajia kupata Sh milioni 90 ili zisaidie ujenzi wa maktaba na jiko katika kituo cha walemavu kilichopo Buhangija mkoa wa Shinyanga,” alisema Fatuma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here