20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

‘Niang bado sana Simba’

??????????????????NA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM

INATIA shaka! Ndivyo unavyoweza kuielezea hatima ya mshambuliaji Msenegali, Papa Niang kusajiliwa na timu ya Simba, kufuatia kuonyesha kiwango kisichoridhisha kwenye mchezo wake wa kwanza ndani ya timu hiyo dhidi ya Mwadui katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana.

Niang aliyewasili nchini Ijumaa iliyopita kusaka ulaji wa kusajiliwa na Simba inayosaka straika hatari wa kufumania nyavu, alicheza kwa dakika 45 tu za kwanza za mchezo huo kabla ya kutolewa kipindi cha pili.

Lakini alionekana kutokuwa fiti mchezoni kuanzia kukimbia hata namna ya kupambana uwanjani, hali iliyowafanya baadhi ya mashabiki wa Simba nao kupata shaka juu ya uwezo wake na kuanza kumponda wakidai bado sana.

MTANZANIA lilifanya jitihada za kumpata Kocha wa viungo wa Simba, Dusan Momcilovic raia wa Serbia baada ya Kocha Mkuu Dylan Kerr kupotea, ambaye alisema kwa ufupi kuwa: “Bado hayupo fiti, hawezi kuwa straika, kukimbia hawezi sidhani kama anaweza kuisaidia Simba, hata kutolewa kwake ilikuwa kwa sababu hiyo. Ila atapewa programu maalumu.”

Moja ya kosa kosa alizofanya Niang kwenye mchezo huo ni dakika ya 5 alipokuwa akitazamana na kipa wa Mwadui, Shabani Kado, lakini beki Joram Mgeveke alimzidi ujanja na kuondoa hatari hiyo.

Simba ilionekana ikicheza bila mipango yoyote ya kusaka bao, eneo lake la ushambuliaji likionekana kupwaya kwa wachezaji kutoelewana vema.

Kocha wa Simba, Dylan Kerr, alianza kwa kuwaanzisha Mwinyi Kazimoto, Awadh Juma na Mzimbabwe, Justice Majabvi, huku kwenye ushambuliaji Niang akicheza sambamba na Mussa Hassan ‘Mgosi’.

Hata baada ya kipindi cha pili Kerr kuwapumzisha Niang na Mgosi na kuwaingiza Hamis Kiiza na Danny Lyanga, bado Simba iliendelea kukosa mabao.

Kiiza mwenyewe akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 58 alipiga shuti dogo lililodakwa vema na Kado, ambaye aliumia dakika ya 77 kwa kugongana na Lyanga wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa shambulizi la Simba, nafasi yake ilichukuliwa na Jackson Abdulazak.

Katika mchezo huo, Simba iliweza kuwatumia makipa wake wote watatu, Muivory Coast, Vincent Angban aliyetoka dakika ya 30 na kuingia kinda Denis Richard, ambaye naye alipumzishwa dakika ya 64 na kuingia Manyika Peter Jr.

Wachezaji wapya wa Mwadui waliocheza Ligi Kuu msimu uliopita, Jerryson Tegete na Nizar Khalfan (wote Yanga) na Paul Nonga (Mbeya City), walioingizwa kipindi cha pili nao walishindwa kuisadia timu hiyo iliyopanda daraja na kutoa sare hiyo.

Hiyo ni sare ya kwanza kwa kocha Kerr tangu aanze kuinoa Simba, kati ya mechi nane za kirafiki alizoiongoza, saba ameibuka na ushindi wa asilimia 100 huku timu hiyo ikifunga mabao 18.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles