28.4 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Diamond azua mjadala mtandaoni

diamond-numzELLY MHAGAMA (TUDARCO)

NYOTA wa muziki Afrika Mashariki na Kati, Nasib Abdul ‘Diamond Platnamuz’, amezua mjadala katika mitandao mbalimbali ya kijamii baada ya kumuunga mkono mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli katika kurasa zake mitandaoni.

Lakini licha ya Diamond kuandika hayo aliomba wachangiaji wasiandike lugha za matusi wakati wa kuchangia mjadala alioanzisha bali aliwataka waandike hoja ili wamshawishi afuate chama chao.

“Msijisumbue kuandika matusi kwa kuwa kila mtu ana haki ya kuchagua kiongozi anayefaa, anayeamini ni bora, mchapakazi, mwenye afya na msimamo ili kutuendelezea nchi yetu, unapohisi una cha kumtetea umtakaye karibu uniambie hapo na mimi nikumwagie zangu ili pamoja tujenge nchi,” aliandika Diamond.

Msanii huyo alikua mmoja wa wasanii walioshiriki kutumbuiza kwenye uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Viwanja vya Jangwani jana, wasanii wengine ni Bushoke, Yamoto Bendi, Ruby na wengine wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles