23.8 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Ray C kufanya shoo Kenya mwishoni mwa wiki

ray-cMWANAMUZIKI aliyepitia changamoto za matumizi ya dawa za kulevya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, mwishoni mwa wiki anatarajiwa kufanya onyesho nchini Kenya.

Onyesho hilo la kumrudisha mwanadada huyo aliyewahi kujizolea umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa kukata kiuno na kuimba litafanyika katika mji wa Malindi.

Umbo na uwezo wake wa kunengua kwa madoido na sauti nzuri aliyokuwa nayo ndivyo vilivyompa umaarufu kwa idadi kubwa ya wapenda burudani nchini Kenya, Uganda na Tanzania.

Lakini hata hivyo, muda aliotumia katika nyumba ya kutunzia wanaotumia dawa za kulevya ulibadilisha umbo lake ambalo wengi wanataka kuona namna anavyoweza kulitumia wakati atakapokuwa akiimba kama atakuwa kama alivyokuwa zamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles