32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

ORCI YAONGEZA MUDA WA KUTOA TIBA YA MIONZI

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) imeongeza muda wa kutoa tiba ya mionzi hadi usiku kutokana na changamoto iliyojitokeza ya kuharibika kwa mashine moja ya tiba ya mionzi (EQ80).

Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dk. Julius Mwaiselage amesema hayo leo Jumamosi alipozungumza na Mtanzania Digital na kuongeza kuwa taasisi hiyo ina mashine nne za tiba ya mionzi ambapo mbili ni za tiba mionzi EQ80 na EQ100 na mbili za tiba mionzi kwa ndani (brachytherapy).

“Mashine ya EQ80 iliharibika ͚’driveshaft͛’ ya kitanda ambayo huendesha kupanda na kushuka kwa kitanda chake Februari, mwaka huu saa sita mchana, mafundi wa taasisi walinunua kipuri hicho wakatengeneza ikafanya kazi hadi Februari 28, mwaka huu ambapo kifaa hicho kiliharibika tena,” amesema.

Amesema jitihada za kupata kipuri kipya kutoka kiwandani nchini Canada zinaendelea na kwamba wanatarajia kitawasili nchini wiki ijayo.

“Mashine ya EQ100 inaendelea kufanya kazi kama kawaida hivyo Taasisi imeongeza muda wa kufanya kazi kwa saa 24 ili kuhakikisha wagonjwa wote wanatibiwa,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles