28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Ommy Dimpoz: Wema siyo mpenzi wangu

wemaNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amesema anashangazwa na uvumi unaoendelea kuwa yupo katika uhusiano na mwigizaji wa filamu, Wema Sepetu.
Akielezea kuhusu picha zilizosambaa kwenye mitandano ya kijamii, Ommy Dimpoz, alisema walikuwa Afrika Kusini kwa mapumziko ndipo picha hizo zilipopigwa.
“Tunapiga picha nyingi sana na Wema, hii siyo mara ya kwanza, lakini sijui kwanini hizi zimetengeneza taswira nyingine kwa mashabiki,” alisema.
Picha za wawili hao wakiwa katika pozi tofauti zimeendelea kuwa gumzo na kuzua maswali mengi kwa mashabiki, kutokana na ukaribu aliyonao Ommy Dimpoz na aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Wema, Nasib abdul ‘Diamond’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles