25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Ole Sendeka awa msemaji wa CCM

Christopher ole SendekaNA CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Mbunge wa zamani wa Simanjiro mkoani Manyara, Christopher ole Sendeka kuwa msemaji wa chama hicho.

Ole Sendeka atafanya kazi za Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo hadi Juni mwaka huu baada ya Halmshauri Kuu kufanya vikao vyake.

Katibu Mkuu wa Chama hicho, Abdulrhaman Kinana aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa Sendeka atashika wadhifa huo hadi   Halmashauri Kuu ya CCM itakapokaa na kuijadili nafasi hiyo katika kikao kitachofanyika Juni mwaka huu.

Kinana alisema katika kikao kitakachofanyika Juni, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete anatarajiwa kukabidhi mikoba ya nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho kwa Rais  Dk.John Magufuli kama ilivyo kawaida.

Alisema tayari chama kimefanya mazungumzo na Dk.Magufuli na ameridhia kushika wadhifa huo na tarehe rasmi ya shughuli hiyo muhimu itapangwa na halmashauri kuu ya chama hicho.

“Kutokana na msemaji wetu Nnauye kuteuliwa kuwa waziri nafasi yake ndani ya CCM kwa sasa itashikwa na Sendeka hadi hapo halmashauri ya chama chetu itakapokaa kujadili nafasi hiyo kwa kuwa wao ndiyo wenye mamlaka,”alisema Kinana.

Alisema hatua hiyo imechukuliwa kumpa nafasi  Nnauye kuendelea na majukumu yake ya uwaziri huku pia wakisubiri atakayechaguliwa kushika wadhifa huo.

Kinana pia alizungumzia taarifa mbalimbali, malalamiko kwenye mitandao ya  jamii kuhusiana na wanachama waliojitangaza kujivua nyadhifa ndani ya CCM  katika Uchaguzi Mkuu uliopita lakini wameanza kurejea ndani ya chama hicho.

“Kumekuwa na mijadala mingi kwenye mitandao ya  jamii kuhusiana na wanaoanza kurejea ndani ya CCM ambao walitoka katika uchaguzi Mkuu uliopita… ukweli ni kwamba wanaorejea ni wengi hadi sasa lakini kikubwa kinachozua mijadala ni baada ya kuona wenye majina makubwa nao wameanza kurejea,”alisema Kinana.

Alisema chama hicho kina mfumo wa kupokea wanachama wapya lakini kwa wale wanaorejea  na kuongeza kuwa ipo haja ya kutengeneza mfumo upya   kuondoa malalamiko yanayojitokeza hivi sasa.

“Kama chama tangu mwanzo hatukuwa na utaratibu mzuri wa kuwabana waliojitoa kisha kurejea hivyo inatakiwa kama chama tukae upya na kupanga utaratibu wa kupokea wanachama hasa wale waliojiondoa kwa kebehi na ubinafsi itafutwe namna ya kuwapokea,”alisema Kinana.

Mwishoni mwa wiki iliyopita kada wa chama hicho na Waziri wa Katiba na Sheria wa zamani Balozi Juma Mwapachu alitangaza kurejea ndani ya chama hicho ambacho alijiondoa siku chache kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana.

Hata hivyo, Mwapachu hakuwahi kujiunga na chama chochote cha siasa hadi alipotangaza tena kurejea kwenye chama chake cha awali.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles