OFISI ya Chama cha Republican katika jimbo la North Carolina imeharibiwa na moto baada ya kitu kinachodhaniwa kuwa bomu lililotengenezwa kienyeji kurushwa ndani ya ofisi hiyo huku jengo lililo karibu yake likipakwa rangi ya nembo inayopinga chama hicho.
Chama hicho kimesema chupa iliyojazwa mafuta yanayoweza kushika moto ilirushwa katika dirisha la makao makuu ya chama cha Republican iliyoko eneo la Orange.
Mkurugenzi wa Republican, Dallas Woodhouse, alisema hakuna mtu aliyejeruhiwa na kwamba tahadhari ya usalama imetumwa katika ofisi nyingine za chama hicho.
”Wanachama wa Nazi walio katika chama cha Republican ni sharti waondoke mjini,” alitahadharisha Woodhouse.
Mgombea Urais wa Cmama cha Democrat, Hillary Clinton ameandika katika mtandao wake wa Twitter kwamba shambulio hilo ni ”la kutisha na halikubaliki.”
Mgombea Urais wa Chama cha Republican, Donald Trump, alionekana akiwalaumu wafuasi wa Democrat kwa kutekeleza kitendo hicho.
”Wanyama wanaomwakilisha Hillary Clinton huko North Carolina walirusha bomu katika ofisi yetu ya Orange kwa sababu wanajua tutashinda,” alisema Trump katika mtandao wake wa Twitter.