30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Odom aanza kunywa pombe

lamar odomLOS ANGELES, MAREKANI

NYOTA wa zamani wa kikapu, Lamar Odom, ameanza kunywa pombe kwa mara ya kwanza tangu atoke hospitali, ambako alipelekwa kutokana na kuathirika na dawa za kulevya.

Mchezaji huyo alipelekwa hospitali Oktoba mwaka jana, baada ya kupoteza fahamu kutokana na kuathirika na matumizi ya madawa ya kulevya.

Hata hivyo, nyota huyo baada ya kutoka hospitalini aliambiwa apunguze matumizi ya pombe, lakini mwishoni mwa wiki hii ameonekana akinywa pombe katika kusherehekea Sikukuu ya Pasaka.

Odom alikuwa na mpenzi wake, Khloe, lakini mchezaji huyo alionekana kuwakimbia waandishi wasiweze kumpiga picha huku akiwa na pombe.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles