27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

50 Cent ajitoa kwenye Instagram

50_centNEW YORK, MAREKANI

RAPA 50 Cent amedai kujitoa kwenye mtandao wa Instagram kutokana na baadhi ya mashabiki kufungua akaunti mbalimbali kwa ajili ya kulichafua jina lake.

Bosi huyo wa kundi la G-Unit, amesema kwamba wapo mashabiki wanafungua akaunti za Instagram wakitumia jina la  50 Cent halafu wanaweka picha mbalimbali za ajabu.

“Sioni sababu ya kuendelea kuwa kwenye Instagram kutokana na baadhi ya watu kuutumia vibaya mtandao huo, kuna watu wanafungua akaunti na kuweka picha zangu na mambo mengine ambayo hayana maana yoyote kwa jamii.

“Kuanzia sasa yeyote ambaye ataona picha zangu kwenye Instagram, siyo mimi, ni baadhi ya watu wanaotaka kulichafua jina langu, lakini wafanyakazi wangu ambao ni wataalamu wa kompyuta wanafanya utafiti kuweza kumjua mhusika,” aliandika 50 Cent kwenye akaunti yake ya Twitter.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles