29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

Mona Star kuachia video mpya

NA MWANDISHI WETU

CHIPUKIZI wa muziki wa kizazi kipya anayetamba na kibao chake cha ‘Hono’, Muona Mwamsumbwe, maarufu kama Mona Star, atatoa video yake ya wimbo huo baadaye mwezi huu.

Akizungumza na gazeti hili wakati akijiandaa kuachia video hiyo, Mona alisema kibao hicho ambacho kinatamba katika vituo mbalimbali vya redio, amekiimba katika mahadhi ya mduara na kwamba anatarajia itapokewa vizuri na mashabiki wake.

“Video imetengenezwa na kampuni ya Blue Sky yenye maskani yake Tabata, imefanya vizuri sana kwa kweli na nadhani ni miongoni mwa kazi nzuri zilizofanywa nyumbani. Ninawaomba mashabiki wanisapoti kwa kuiomba kwenye vituo vye televisheni ili waone ubora,” alisema msanii huyo, ambaye pia anatamba na nyimbo zake nyingine za ‘Narejea’ na ‘Hatufanani’.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles