27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Obi Mikel atangaza kuondoka Chelsea

mikel-udeytrymediaLONDON, ENGLAND

KIUNGO wa timu ya Chelsea, Obi Mikel, ameweka wazi kwamba baada ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu nchini England ataondoka katika klabu hiyo.

Mkataba wa mchezaji huyo unatarajia kumalizika 2017, lakini amedai kuwa kukosa katika nafasi ya kwanza mara kwa mara kunamfanya atafute timu ambayo atapata nafasi ya kuonesha uwezo wake.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28, raia wa Nigeria, amesema anachukizwa na kuwekwa benchi kwa kuwa kiwango chake kitapotea.

“Kwa sasa nimebakisha msimu mmoja kuweza kumaliza mkataba wangu, lakini ninaelewa baada ya ligi kumalizika klabu inaangalia nini ilikosea na nini kifanyike, ila kama wakisema niondoke niko tayari na kama wakisema natakiwa kuendelea kuwepo basi lazima wahakikishe napata namba katika kikosi cha kwanza.

“Kitu ambacho nakichukia katika maisha yangu ni kuwekwa benchi kama inavyofanyika katika klabu hii, hakuna mchezaji ambaye anapenda kukaa nje ya uwanja bila kucheza, hivyo lazima niondoke kama hali itakuwa hivyo,” alisema Mikel.

Mchezaji huyo alikuwa wa akiba wakati wa Kocha Jose Mourinho, kabla ya kocha huyo kufukuzwa Desemba mwaka jana, lakini mchezaji huyo alianza kupata nafasi baada ya ujio wa kocha wa muda, Guus Hiddink.

Hata hivyo, mchezaji huyo anaamini kuwa hali ya kukaa benchi itaendelea endapo atakuja kocha mpya, tayari klabu hiyo imefanya mazungumzo na kocha wa timu ya Taifa ya Italia, Antonio Conte kwa ajili ya mkataba wa miaka mitatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles